Saturday, December 7, 2013

SUAREZ ANA THAMANI ZAIDI YA PAUNDI MILIONI 70 - HAMANN.

KIUNGO wa zamani wa klabu ya Liverpool, Dietmar Hamann anafikiri kuwa paundi milioni 71 hazitoshi kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji nyota wa timu hiyo Luis Suarez. Klabu ya Real Madrid inajiandaa kumnyakuwa nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwakani na wako tayari kulipa kitita cha paundi milioni 70. Hata hivyo Hamann ambaye amecheza Liverpool kwa miaka saba anafikiri kuwa nyota huyo ana thamani zaidi ya hiyo kwasababu ya kiwango alichokionyesha msimu huu akiwa amefunga mabao 13 katika mechi tisa alizocheza. Hamann ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani pia ameionya Liverpool kuwa inaweza kumkosa nyota huyo kama wakishindwa kujihakikishia nafasi ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment