Saturday, December 7, 2013

TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA MWAKANI KUINGIA SOKONI DESEMBA 8.

TIKETI kwa ajili ya michuano ijayo ya Kombe la Dunia zinatarajiwa kuanza kuuzwa Desemba 8 huku tiketi kwa ajili ya mechi zote zikiwepo kasoro za mechi ya ufunguzi kati wenyeji Brazil na Croatia utakaofanyika jijini Sao Paulo na za fainali itakayofanyika jijini Rio de Janeiro katika Uwanja wa Maracana. Katika taarifa yake iliyotumwa katika mtandao, Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lilidai kuwa tiketi hizo zitaanza kuuzwa kuanzia Desemba nane na kumaliza zoezi hilo ifikapo Januari 30 mwakani. Baada ya ratiba kamili ya michuano hiyo kupangwa jana mashabiki sasa wanaweza kununua tiketi hizo kwa mechi husika wanazozihitaji. Kwa upande wa Tanzania, Shirikisho la Soka la hapa-TFF limepewa tiketi 260 na watanzania wapenzi wa soka watakaohitaji kwenda kushuhudia michuano watatakiwa kutuma maombi yao ya maandishi kwa ajili ya kununua tiketi hizo.

No comments:

Post a Comment