Saturday, December 7, 2013

PELE AITABIRIA BRAZIL KUFIKA FAINALI KOMBE LA DUNIA.

NGULI wa soka Brazil, Pele ameitabiria nchi yake kufika fainali katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 kufuatia droo ya makundi iliyopangwa Ijumaa. Katika droo hiyo Brazil ambao wako katika kundi A na timu za Croatia, Mexico na Cameroon. Kikosi cha Brazil ambacho kinanolewa na Luiz Felipe Scolari kitacheza mechi yake ya ufunguzi na Croatia Juni 12 katika mji wa Sao Paulo lakini kama wakifanikiwa kutinga hatua ya timu 16 bora wanaweza kukwaana na timu ngumu kama Hispania, Uholanzi, Chile au Australia. Hata hivyo Pele akihojiwa kuhusiana na hilo amesema ana uhakika Brazil itatinga fainali. Pele amesema anakumbuka baba yake alivyolia machozi baada ya kulikosa Kombe la Dunia mwaka 1950 hivyo hataki watoto wake wamuone akilia kama wakilikosa.

No comments:

Post a Comment