Tuesday, December 10, 2013

WAZIRI WA MICHEZO UTURUKI AWATETEA KINA DROGBA.

WAZIRI wa michezo wa Uturuki amepinga uamuzi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo kuwaadhibu wachezaji wawili wa kimataifa wa Ivory Coast wanaocheza katika klabu ya Galatasaray kwa kutoa heshima zao kwa Nelson Mandela aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita. Didier Drogba na Emmanuel Eboue wametishiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu na shirikisho hilo kwa kukiuka masharti ya kuvaa fulana iliyokuwa na maandishi yanayohusiana na mambo ya kisiasa. Waziri huyo Suat Kilic amelitaka shirikisho hilo kuangalia upya uamuzi wake dhidi ya wachezaji hao. Kilic amesema haoani kama uamuzi wowote wa kuwaadhibu wachezaji hao utaleta picha nzuri kwa nchi hiyo kwasababu wataonekana kama wamenyimwa haki yao ya kuwasilisha mawazo yao hususani katika kipindi hiki ambacho dunia nzima inamuenzi kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment