Tuesday, December 10, 2013

CELTIC YAWAFUNGIA MASHABIKI WAKE KWA UHARIBIFU.

KLABU ya Celtic ya Scotland imewafungia mashabiki wake 128 kuhudhuria mechi zake za nyumbani na ugenini wakati uchunguzi ukielendelea kufuatia uharibifu uliofanyika katika Uwanja wake wa Fir Park uliopo katika kitongoji cha Motherwell. Katika tukio hilo viti vilivunjwa na mashabiki na polisi waliokuwepo uwanjani wanadai kuwepo kwa mafataki na mabomu ya moshi na gesi wakati wa mchezo huo ambao Celtic walishinda kwa mabao 5-0. Katika taarifa yake iliyotumwa katika mtandao klabu hiyo imedai kuwa tukio hilo ni la aibu kwa timu kubwa kama hiyo na hawawezi kulifumbia macho hivyo ni lazima wachukue hatua kali kwa wahusika. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa timu hiyo haiwezi kuwaruhusu watu wachache kuharibu jina zuri walilokuwa nalo katika mchezo huo unaopendwa dunia nzima.

No comments:

Post a Comment