Friday, January 10, 2014

AUSTRALIA OPEN 2014: SERENA WILLIAMS KUANZA BARTY.

MCHEZAJI tenisi nyota anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani Serena Williams anatarajiwa kuchuana na Ashleigh Barty katika mchezo wa mzunguko wa michuano ya wazi ya Australi wiki ijayo. Katika ratiba hiyo iliyopangwa jana Williams anatarajiwa kukutana na kigingi katika kama akifika mzunguko wan ne ambapo anaweza kuchuana na Samantha Stosur aliyemfunga katika michuano ya wazi ya Marekani mwaka 2011. Bingwa mtetezi wa michuano hiyo Victoria Azarenka anatarajiwa kucheza na Johanna Larsson wa Sweden. Mwanadada Maria Sharapova anayeshika nafasi ya tatu katika orodha hizo anatarajiwa kuanza na Bethanie Mattek-Sands wakati Li na anayeshika nafasi ya nne atachuana na mmojawapo ya wachezaji waliofuzu.

No comments:

Post a Comment