RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amependekeza kutumika kwa adhabu ya muda ikiwa ni njia mojawapo ya kudhibiti suala la kujirusha katika soka. Blatter anafikiri kuwa wachezaji ambao wanapatiwa matibabu lakini hawajaumia sana wanatakiwa kusubirishwa kwa muda zaidi kabla ya hajaruhusiwa kurejea uwanjani kucheza tena. Blatter mwenye umri wa miaka 77 amesema ni jambo la kuudhi kwa mchezaji kujifanya kaumia sana mpaka anakaribia kufa halafu baada ya muda kidogo toka wamtoe anarejea tena uwanjani kama ahakuna lililotokea. Blatter aliendelea kudai kuwa mwamuzi anaweza kuamua kumuweka mchezaji nje mpaka timu yake ianze kupata athari ndipo amuingize ili matukio hayo yasiwe yakijirudia mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment