KAMATI ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2022 itakayofanyika nchini Qatar imedai kuwa nchi hiyo iko tayari kuandaa michuano hiyo kwa muda wowote kama ni kipindi cha majira ya joto au baridi. Kwasasa Shirikisho la Soka Dunia-FIFA limeandaa kikosi kazi kitakachojadili uwezekano wa kuhamisha michuano hiyo ichezwe katika majira ya baridi kutokana na joto kali katika nchi hiyo kwenye majira ya kiangazi. Hata hivyo msemaji wa kamati hiyo Al-Khater amesema mipango yao ni kuandaa michuano hiy katika kipindi cha majira ya kiangazi kama walivyoahidi hivyo wanasubiri uamuzi wa jumuiya wa michezo ya kimataifa itakavyoamua na tarehe yoyote watakayokubaliana wao wako tayari. Al-Khater amesema tayari ujenzi wa uwanja wa kwanza utakaotumika kwa ajili ya michuano hiyo umeshaanza kujenga na vingine vitano zaidi vitaanza ujenzi wake baadae mwaka huu. Al-Khater aliendelea kudai kuwa malengo yao ya kuweka vipoza hewa sio kwajili ya viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo pekee bali hata sehemu mbalimbali zitakazokuwa na mkusanyiko wa watu ikiwemo na kambi za mashabiki.
No comments:
Post a Comment