WAZIRI wa michezo wa Cameroon, Adoum Garoua ametangaza ujenzi wa viwanja viwili vipya kuelekea michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019 ambapo nchi hiyo inategemea kuwa mwenyeji baada ya kutuma maombi ya kuandaa michuano hiyo Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF. Kampuni moja ya China imepewa tenda ya kuandaa michoro ya viwanja viwili ambao utajumuisha mmoja wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 katika wilaya ya Olembe katika mji mkuu wa nchi hiyo Yaounde. Waziri huyo amesema viwanja vilivyopo jijini Yaounde, Douala na Garoua vitafanyiwa ukarabati ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali kufanyia marekebisho miundo mbinu ya michezo. Cameroon imewahi kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika mara moja pekee mwaka 1972 ambapo Congo walinyakuwa taji hilo.
No comments:
Post a Comment