RAIS wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesisitiza kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumbadilisha Franck Ribery kwa ajili ya kumsajili Cristiano Ronaldo. Ribery alimaliza katika nafasi ya tatu katika kinyang’anyiro cha Ballon d’Or 2013 ambapo Ronaldo alinyakuwa tuzo hiyo akifuatiwa na Lionel Messi aliyeshika nafasi ya pili. Rummenigge amesema hakushangazwa na Ronaldo kupewa tuzo hiyo lakini akasisitiza kuwa Ribery atabakia mchezaji mwenye thamani zaidi na hawezi kumbadilisha kwa ajili ya Ronaldo. Rais huyo pia amesema watafanya kila wawezalo ili kuhakikisha wanawabakisha nyota wao Mario Mandzukic na Arjen Robben baada ya kuzuka tetesi kuwa wanaweza kutimka mwishoni mwa msimu.

No comments:
Post a Comment