JOTO kali lililopo katika jiji la Melbourne limesababisha kusimamishwa kwa michuano ya tenisi ya wazi ya Australia kwa masaa manne. Baadhi ya michezo ambayo ilikuwa ichezwe katika viwanja vya wazi ilishindikana kutokana na joto kuzidi na kufikia nyuzi joto 43 hatua ilipelekea waandaaji kusogeza mbele mpaka muda wa jioni ambao joto huwa linapoa kidogo.
Pamoja na baadhi ya viwanja kusimama lakini viwanja vingine katika michuano hiyo kama Rod Laver Arena na Hisense mechi zake ziliendelea kama kawaida baada ya kufunikwa juu ya paa na kuwashwa vipoza hewa. Jumanne waandaji wa michuano hiyo walishambuliwa kwa kuruhusu wachezaji kucheza katika joto kali hatua iliyopelekea wengine kuzidiwa na kuanguka.


No comments:
Post a Comment