Wednesday, January 15, 2014

PELLEGRINI ATAMBA KUNYAKUWA MATAJI YOTE MANNE UINGEREZA.

MENEJA wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesema anataka kuweka alama katika msimu wake wa kwanza Uingereza kwa kushinda mataji yote manne wanayoshindania. City kwasasa wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu huku wakiongoza kwa mabao 6-0 katika mchezo wa nusu fainali mkondo wa kwanza Kombe la Ligi dhidi ya West ham United na wataikabili Barcelona katika hatua ya timu 16 bora kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akihojiwa kabla ya mchezo wao wa leo wa Kombe la FA mzunguko wa tatu dhidi ya Blackburn Rovers, Pellegrini amesema anajua ni ngumu kushinda mataji yote manne lakini ni muhimu kujaribu. Hakuna klabu yoyote Uingereza iliyoweza kushinda mataji ya Ligi Kuu, Ligi Mabingwa Ulaya, Kombe la FA na Kombe la Ligi. Majirani Manchester United ndio walioweza kunyakuwa mataji matatu ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA msimu wa 1998-1999 lakini walichemsha kuchukua Kombe la Ligi baada ya utolewa na Tottenham katika hatua ya robo fainali.

No comments:

Post a Comment