MWANADADA Serena Williams amefanikiwa kutinga mzunguko wa tatu katika michuano ya wazi ya Australia kwa kumgaragaza Vesna Dolonc pamoja na joto kali lililopo katika jiji la Melbourne. Michuano hiyo safari imekumbwa na joto kali katika eneo hilo linalofikia nyuzi joto 42 hivyo kupelekea baadhi ya wachezaji kushindwa na wengine kuanguka na kushindwa kuendelea na mchezo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Williams ambaye alimfunga Dolonc kwa 6-1 6-2 amesema hali ya joto ilikuwa ikimtia hofu lakini anashukuru kwa kufanikiwa kushinda mechi hiyo na kusonga mbele. Hali ya joto imekuwa ikilalamikiwa na wachezaji wengi ambapo mwanadada Victoria Azarenka amedai kuwa kucheza katika joto hilo ni sawa na kama upo katika chungu cha moto wakati Frank Dancevic wa Canada aliwaponda waandaaji kwa kukubali wachezaji katika hali hiyo mbaya.

No comments:
Post a Comment