Wednesday, January 15, 2014

RAFAEL AKANUSHA KUTAKA KUONDOKA UNITED.

BEKI wa klabu ya Manchester United, Rafael amepinga madai yaliyotolewa na wakala wake kuwa anaweza kuondoka Old Traford katika kipindi cha majira ya kiangazi. Cassiano Pereira ambaye ni wakala Mbrazil huyo na pacha wake Fabio alikaririwa akidai kuwa kuna uwezekano wa mteja wake kuondoka kiangazi. Lakini nyota huyo aliwaondoa mashabiki wa timu hiyo hofu kwa kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa hana mpango wa kuondoka. Toka kuanza kwa msimu Rafael amecheza mechi tisa pekee za ligi huku akitokea benchi mechi tano kati ya hizo. Pacha wake Fabio amekuwa akihusishwa na kuhamia katika klabu ya Cardiff City katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha meneja mpya David Moyes.

No comments:

Post a Comment