Thursday, January 16, 2014

KESI YA POWELL YAPIGWA KALENDA.

BINGWA wa zamani aliyekuwa akishikilia rekodi yam bio za mita 100, Asafa Powell anatarajia kusubiri hatma mpaka Februari 12 mwaka huu kama atafungiwa kukimbia kwa miaka miwili. Powell raia wa Jamaica anatuhumiwa kutumia madawa yaliyokatazwa ya oxilofrine lakini kesi yake iliahirishwa Jana mpaka tarehe hiyo iliyotajwa. Katika utetezi wake wakala wa Powell alimtupia lawama mkufunzi wake Chris Xuereb kwa kumpa dawa hizo bila kuwa na taarifa. Powell ambaye aliweka rekodi ya dunia kwa kutmia sekunde 9.74 mwaka 2007 ni mmoja kati ya wanariadha watano wa Jamaica waliopimwa na kukutwa na chembechembe za dawa hizo juni mwaka jana akiwa pamoja na mwanadada Sherone Simpson ambaye naye mkufunzi wake ni Xuereb.

No comments:

Post a Comment