Thursday, January 16, 2014

TANZANIA YAKWEA TENA VIWANGO FIFA.

TANZANIA imefanikiwa kupanda tena katika viwango vya ubora vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Katika viwango vilivyotolewa mwezi huu Tanzania imekwea kwa nafasi mbili mpaka nafasi ya 118, ukilinganisha viwango mwa Desemba mwaka jana ambapo alikuwa katika nafasi ya 120. Mwezi huu kumekuwa hakuna mabadiliko sana katika orodha hiyo ambapo mabingwa wa Dunia na Ulaya Hispania imeendelea kuongoza wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Argetina. Wengine katika tano bora ya orodha hiyo ni Colombia waliopo nafasi nne wakifuatiwa na Ureno katika nafasi ya tano. Kwa upande wa Afrika nako kuna mabadiliko machache ambapo Ivory Coast wameendelea kuongoza kwa kung’ang’ania nafasi yao ya 17 wakifuatiwa na Ghana waliopo nafasi ya 24 wakati Algeria wao wameanguka kwa nafasi moja mpaka nafasi ya 27.Nafasi ya nne na tano kwa upande wa Afrika kumekuwa na ingizo jipya ambapo Misri wamekwea katika nafasi hiyo baada ya kupanda kwa nafasi 10 mpaka ya 31 wakifuatia na Cape Verde waliopanda kwa nafasi nne mpaka 35.

No comments:

Post a Comment