Saturday, January 18, 2014

GUARDIOLA AKIRI KUKABILIWA NA MECHI NGUMU.

MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amekiri kukitegemea kikosi chake chote wakati watakapoingia katika mechi ngumu katika harakati zao za kujaribu kushinda mataji yote matatu kwa mara nyingine. Mabingwa hao watetezi wa Bundesliga na Ligi ya Mabingwa Ulaya wanatarajia kurejea tena uwanjani baada ya mapumziko ya majira ya baridi Januari 24 watakapokwaana na Borussia Monchengladbach. Mechi hiyo itakuwa ni mojawapo kati ya mechi sita mfululizo watakazocheza ndani siku 18 kabla hawajakutana na Arsenal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya mtoano. Akihojiwa katika mazoezi yao huko Doha, Qatar, Guardiola amesema wana kikosi kikubwa huku wakikabiliwa na mechi nyingi katika kila siku tatu hivyo anahitaji kila mchezaji katika kikosi chake.


No comments:

Post a Comment