MENEJA wa klabu ya Paris Saints-Germain, PSG Laurent Blanc amebainisha kuwa hawana mpango wa kumsajili Lionel Messi kwasababu malengo yao ni kuboresha sehemu ya kiungo. PSG imekuwa ikihusishwa kwa kipindi kirefu na suala la kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina kwa ada ya kuvunja rekodi inayaokadiriwa kufikia euro milioni 250. Hata hivyo Blanc alipuuzia uvumi huo na kueleza kuwa kwasasa mpango wao ni kuongeza nguvu katika safu ya kiungo huku tetsi zikizidi kuzagaa huenda wakamchukua Paul Pogba kutoka klabu ya Juventus ya Italia. Kumekuwa na tetesi kuwa PSG wanajiandaa kumtoa sadaka Marco Virratti ili waweze kumpata Pogba wakati nyota wa Chelsea Juan Mata na Eden Hazard nao wakiwa katika rada zao.

No comments:
Post a Comment