Saturday, January 18, 2014

AUSTRALIA OPEN: FEDERER, MURRAY, SHARAPOVA WASONGA MBELE.

MICHUANO ya tenisi ya wazi ya Australia imeendelea leo jijini Melbourne ambapo nyota kadhaa wanaoshika nafasi za juu katika orodha za ubora duniani wameendelea kung’ara kwa kushinda mechi zao na kutinga hatua ya mzunguko wa nne. Kwa upande wa wanaume Mwingereza Andy Murray alifanikiwa kusonga mbele kwa kumfunga kirahisi Feliciano Lopez wa Ufaransa kwa seti 3-0 zenye alama za 7-6 6-4 6-2 ambapo sasa atakwaana na Stephane Robert. Naye bingwa mara 17 wa Grand Slam kutoka Switzerland, Roger Federer amefanikiwa kusonga mbele baada ya kumgaragaza Teymuraz Gabashivili wa Urusi kwa kwa seti 3-0 zenye alama za 6-2 6-2 6-3. Kwa upande wa mwanadada nyota kutoka Urusi Maria Sharapova amefanikiwa kutinga katika mzunguko wa nne kwa kumfunga Alize Cornet wa Ufaransa kwa 6-1 7-6 ambapo sasa atakwaanza na Dominika Cibulkova wa Slovakia katika kinyang’anyiro cha kutinga robo fainali.

No comments:

Post a Comment