Saturday, January 18, 2014

OZIL AMUANGUKIA WENGER ASAINI MKATABA MPYA.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil amesisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha Arsene Wenger anasaini mkataba mpya kwasababu kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 ana uwezo kusukuma wachezaji kucheza katika viawango vyao vya juu. Mkataba wa sasa wa Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu huu lakini tayari kumeshafikiwa makubaliano ya kumuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili ingawa Mfaransa huyo bado ameweka pembeni suala hilo. Kwasasa Arsenal wako kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza kwa tofauti ya alama moja na Ozil anaamini kuwa Wenger ni sehemu muhimu katika kuhakikisha timu hiyo inanyakuwa taji msimu huu. Ozil amesema Wenger ndio aliyemshawishi kujiunga nao kwasababu ni meneja wa kiwango cha juu na anaweza kuisukuma timu kufikia uwezo wa juu na pia wachezaji wanakuwa vizuri wakiwa chini yake.

No comments:

Post a Comment