Saturday, January 18, 2014

CHAN 2014: ETHIOPIA, MSUMBIJI ZAFUNGISHWA VIRAGO.

TIMU ya taifa ya Ethiopia imekuwa timu ya pili kuenguliwa katika michuano ya Mataifa ya Afrika wa wachezaji wa ndani ya bara hili baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Congo kwenye mchezo wa kundi C uliochezwa katika Uwanja wa Free State jijini Bloemfontein. Ethiopia ilitegemewa kuwa mojawapo ya timu ngumu katika michuano hiyo inayojulikana kama CHAN lakini kipigo cha pili mfululizo kinamaanisha kuwa timu haina nafasi ya kuibuka katika nafasi mbili za juu kwenye kundi lao. Timu ya kwanza kuyaaga mashindano hayo ilikuwa ni Msumbiji baada ya wao pia kukubali vipigo mfululizo katika kundi mechi zake za kundi A dhidi ya Wenyeji Afrika Kusini na Nigeria. Michuano hiyo inaendelea tena baadae jioni hii ambapo katika mchezo wa kwanza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC itakwaana na Gabon ambapo yoyote atakayeshinda ndiye atakayeongoza kundi D. Mechi nyingine itakayochezwa usiku itazikutanisha timu za Burundi ambayo ina alama moja baada ya kutoa sare mchezo wake wa kwanza itachuana na Mauritania ambao bado hawana alama yoyote baada ya kufungwa kwenye mchezo wao wa kwanza.

No comments:

Post a Comment