Sunday, January 19, 2014

SERENA WILLIAMS AAGA MICHUANO YA AUSTRALIA OPEN.

MWANADADA nyota wa tenisi Serena Williams ameenguliwa katika michuano ya wazi ya Australia baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Ana Ivanovic wa Serbia. Katika mchezo huo Williams alianza vyema lakini alijikuta akishindwa kumudu vishindo vya Ivanovic kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya mgongo na kujikuta akichapwa seti 2-1 zenye alama za 4-6 6-3 6-3. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Williams amesema ilibaki kidogo ajiengue kucheza kutokana na maumivu ya mgongo yaliyokuwa yakimsumbua lakini akadai hawezi kulaumu chochote kwasababu ni mpambanaji. Williams pia alimsifu mpinzani wake Ivanovic kwa kutumia vyema udhaifu wake na kuhakikisha anashinda mchezo huo.

No comments:

Post a Comment