Sunday, January 19, 2014

MAN UNITED BADO TIMU KUBWA DUNIANI - MOYES.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amepuuza madai kuwa timu hiyo haigopeki kutokana na kuanza msimu kwa kusuasua na kusisitiza kuwa bado ni klabu kubwa duniani. United ambao ni mabingwa wa tetezi wa Ligi Kuu nchini Uingereza wameshindwa kuonyesha cheche zao na kujikuta wako mbali katika mbio za ubingwa huku wakiwa katika hatari ya kukosa nafasi nne za juu ambazo zitawafanya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Akikaririwa na gazeti la Daily Mirror la Uingereza, Moyes amesema United sio klabu kubwa nchini humo pekee bali dunia nzima. Moyes amesema baadhi ya matokeo yao yanaweza kuwa yamekwenda kinyume na mategemeo ya mashabiki lakini hilo halimaanishi kuwa klabu hiyo ndio imekwisha. Kocha huyo ana kibarua kigumu baadae leo ambapo timu yake itakuwa ugenini kuchuana na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment