MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amepongeza kikosi chake kwa kufikisha mabao zaidi ya mabao 100 baada ya ushindi wa mabao 4-2 waliopata katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Cardiff City. Akihojiwa Pellegrini amesema anafikiri jambo hilo ni muhimu kwa timu kwasababu sio suala rafiki kufikisha kiwango hicho cha mabao haswa katika kipindi cha katikati ya msimu lakini hilo linamaanisha malengo yao na jinsi timu inavyocheza. City ambao hawajafunga mechi yoyote nyumbani mpaka sasa wamefunga mabao 63 katika mechi 62 za Ligi Kuu walizocheza wakiwa nyuma ya mabao 40 kufikia rekodi ya Chelsea waliyoweka msimu wa 2009-2010 huku wakiwa wamebakiwa na mechi 16. Klabu ya Aston Villa ndio wanaoshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika ligi wakiwa na mabao 128 katika mechi 42 walizocheza katika msimu wa 1930-1931.
No comments:
Post a Comment