MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester United, Wilfried Zaha amepanga kuomba uhamisho kama kocha wa timu hiyo hatamruhusu kusajiliwa kwa mkopo. Mahusiano ya kambi Zaha na United yameingia utata baada ya Cardiff City kuilaumu United kukwamisha uhamisho wa winga huyo. Mapema wiki hii meneja wa Cardiff ambaye amewahi kuichezea United, Ole Gunnar Solskjaer alidai kuwa tayari wameshafikia makubaliano ya kumchukua Zaha kwa mkopo. Lakini Ofisa Mkuu wa United Ed Woodward anaonyesha kukwamisha suala hilo baada ya kuwapasha Cardiff kuwa hawawezi kumchukua nyota huyo kutokana na majeruhi. Zaha amekuwa akitaka kuondoka United kutokana na kushindwa kuwa katika mipango ya Moyes hivyo kujikuta akishindwa kutokeza katika kikosi cha kwa nza cha timu hiyo.
No comments:
Post a Comment