MENEJA wa klabu ya Juventus, Antonio Conte amemponda Paul Pogba hata baada ya kiungo huyo mahiri kufunga bao murua katika ushindi wa mabao 4-2 iliyopata timu hiyo dhidi ya Sampdoria. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Conte amesema nyota huyo kinda angeweza kufanya vizuri zaidi katika mchezo huo kwani mara nyingi amemuona akicheza vyema zaidi hivyo. Kocha huyo amesema siku zote huwaonya wachezaji wake kuwa makini katika muda wote wa mchezo kitu ambacho katika mchezo huo hawakukifanya huku akimnyooshea kidole nyota huyo kwa kucheza chini ya kiwango chake. Ushindi huo umeendelea kuwaweka Juventus kileleni mwa Ligi Kuu nchini Italia kwa tofauti ya alama nane na AS Roma wanaoshika nafasi ya pili.
No comments:
Post a Comment