MWANADADA nyota wa tenisi Maria Sharapova amefungasha virago kama ilivyokuwa kwa Serena Williams baada ya kukubali kipigo kutoka Dominika Cibulkova wa Slovakia katika mechi ya mzunguko wan ne ya michuano ya wazi ya Australia inayoendelea jijini Melbourne. Sharapova raia wa Urusi ambaye aliwahi kushinda michuano hiyo mwaka 2008 alishindwa kutamba mbele ya Cibulkova na kujikuta akichabangwa seti 2-1 zenye alama za 3-6 6-4 6-1 katika mchezo uliopigwa huko Rod Laver Arena. Bingwa mara tano wa michuano wa michuano hiyo Williams wa Marekani naye alitandikwa jana na Ana Ivanovic hivyo kumuacha bingwa mtetezi Victoria Azarenka kuwa mchezaji pekee mwenye mataji mengi makubwa katika michuano hiyo. Akihojiwa Sharapova amesema ulikuwa mchezo mgumu kutokana na kucheza akiwa na maumivu ya nyonga huku akimpongeza mpinzani wake kwa kufanikiwa kusinga mbele.
No comments:
Post a Comment