TIMU ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles wamewafungisha virago wenyeji Afrika Kusini au Bafana Bafana kwa kuitandika kwa mabao 3-1 katika mchezo wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani uliochezwa jijini Cape Town. Ushindi huo umewafanya Nigeria kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi A wakiwa na alama sita nyuma ya Mali ambao wamemaliza kama vinara wa kundi hilo. Kocha wa Bafana Bafana Gordon Igesund amekiri kuwa kikosi chake kimefungwa kihalali na Nigeria na kuongeza kuwa hawana la kujitetea kutokana na hilo. Hata hivyo kocha huyo alipuuza suala la kujiuzulu na kudai kuwa ataendelea kukifundisha kikosi hicho mpaka mkataba utakapomaliza Juni mwaka huu. Michuano hiyo inaendelea tena leo jioni katka kundi B ambapo Burkina Faso itachuana na Zimbabwe huku Morocco wakicheza na Uganda, timu zote zina nafasi ya kusonga mbele kama zikifanikiwa kushinda mechi zao.
No comments:
Post a Comment