VAN GAAL AKIRI TOTTENHAM KUMTAKA.
KOCHA wa timu ya taifa ya Uholanzi, Louis van Gaal amethibitisha kuwa klabu ya Tottenham Hotspurs walimfuata baada ya kumtimua Andres Villas-Boas. Van Gaal mwenye umri wa miaka 62 sambamba na Guus Hiddink na Fabio Capello wote walitafutwa na Spurs kabla kocha wa muda Tim Sherwood hatapewa kibarua cha kuwa kocha kamili wa timu hiyo. Akihojiwa kocha huyo amesema kila mtu anajua hivyo anakiri kuwa ni kweli Spurs walimtafuta lakini hakupenda kufanya kazi kwa wakati mmoja. Van Gaal aliendelea kudai kuwa tatizo la kazi za ukocha ni kuwa wakati una muda mara nyingi nafasi huwa hazipo lakini wakati una kazi ndio nafasi nyingi za kufundisha zinatokea. Pia kocha huyo amekiri kutamani kufundisha soka katika Ligi Kuu nchini Uingereza lakini hilo litakuwa baada ya kumalizika michuano ya Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment