KLABU ya Barcelona imemjumuisha mshambuliaji wake nyota Lionel Messi katika kikosi kitakachoivaa Getafe katika mchezo wa Kombe la Mfalme unaotarajiwa kuchezwa kesho. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alipata majeraha ya kuchanika msuli katika mchezo wa La Liga dhidi ya Real Betis Novemba mwaka jana na toka kipindi hicho amekuwa nje ya uwanja. Messi alikosa mechi ya kwanza ya Barcelona kwa mwaka huu dhidi ya Elche pamoja na kuruhusiwa kucheza na madaktari lakini sasa anaweza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Getafe. Kocha wa Barcelona Gerardo Martino amesema Messi anajisikia vyema na amekuwa akifanya mazoezi bila matatizo hivyo anadhani yuko tayari kucheza.
No comments:
Post a Comment