Tuesday, January 14, 2014

MOYES AWAMENDEA POGBA NA VIDAL.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amefanya mazungumzo na mhusika wa masuala ya usajili wa klabu ya Juventus ya Italia baada ya kupanga kuwasajili Poul Pogba na Arturo Vidal. Moyes alikutana na mjumbe wa bodi wa Juventus, Beppe Marotta baada ya mchezo wa Juventus na Cagliari Jumapili iliyopita na kujadiliana juu ya uwezekano wa aidha kuwasajili wote kati ya wachezaji hao anaowataka sana. 
Baada ya kusafiri hadi Cagliari na kocha wa kikosi cha kwanza, Jimmy Lumsden kushuhudia Juventus wakitoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 4-1 na kuendelea kuongoza msimamo wa ligi ya Italia, Serie A, Moyes aliweka wazi mipango yake ya kusajili kutoka klabu ya Turin.  Lakini hadi anarejea Manchester, alilazimika kukubali kwamba anaweza kumrejesha Pogba pekee Old Trafford na kuhusu Vidal asubiri hadi mwisho wa msimu. Zinedine Zidane aliwahi kusema kuondoka kwa Pogba United miezi 18 iliyopita lilikuwa ni kosa kubwa alilolifanya kocha wa zamani wa klabu hiyo, Sir Alex Ferguson, lakini Moyes anapambana kumrejesha mkali huyo.

No comments:

Post a Comment