NGULI wa soka wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane amesema yuko tayari kuwa kocha mkuu baada ya kufanya kazi kama kocha msaidizi wa Carlo Ancelotti katika klabu ya Real Madrid. Zidane ambaye aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa michezo wa Madrid mwaka 2011, amechagua kuwa msaidizi wa Ancelotti baada ya Muitaliano huyo kutua klabu hapo kuziba pengo la Jose Mourinho aliyetimuliwa katika kipindi cha kiangazi. Kufuatia kupita miezi sita ya kwanza akiwa chiini ya Ancelotti, Zidane amesisitiza kuwa sasa anadhani yuko tayari kujaribu nafasi yake kama kocha mkuu na kuahidi kukitengeneza kikosi chake kuwa chenye kufanya mashambulizi. Zidane amesema ana hamu kubwa ya kupewa nafasi kamili ya ukocha kwasababu anajiona ana mambo mengi yanayoweza kunufaisha timu yoyote itakayomuhitaji. Zidane ambaye ameshinda mataji manane akiwa mchezaji wa Madrid, pia aliwashukuru Ancelotti na rais wa klabu hiyo Florentino Perez kwa kumsaidia katika kipindi chote ambacho amekuwa hapo.
No comments:
Post a Comment