Saturday, January 4, 2014

POLISI KUFANYIA UCHUNGUZI KAMERA ILIYOKUWA KATIKA KOFIA NGUMU ALIYOKUWA AMEVAA SCHUMACHER WAKATI WA AJALI.

WAKAGUZI nchini Ufaransa wanafanyia uchunguzi kamera iliyofungwa katika kofia gumu alilokuwa amevaa dereva nyota wa zamani wa mashindano ya langalanga Michael Schumacher wakati alipopata ajali akiteleza katika barafu. Wahusika wanategemea kamera hiyo inaweza kuwapa mwanga kuhusu tukio hilo la ajali lililotokea katika milima ya Ufaransa. Polisi pia walimhoji mtoto wa kiume wa Schumacher ambaye alishuhudia ajali hiyo. Kwa upande mwingine mashabiki wa nyota huyo wamemiminika nje ya hospitali anapotibiwa na kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa jana huku wakimuombea apone haraka. Madaktari wanamtibu nyota huyo wamedai kumuweka katika dozi nzito ya usingizi ili ubongo wake uweze kujitibu taratibu baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili ili kuondoa damu iliyovuja kwenye ubongo wake.

No comments:

Post a Comment