Saturday, January 4, 2014

HISPANIA KUIVAA ITALIA KABLA YA KWENDA BRAZIL.

MABINGWA wa Dunia na Ulaya timu ya taifa ya Hispania inatarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Italia Machi 5 mwaka huu kabla ya kocha wake Vincente de Bosque hajatangaza kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia. Mechi hiyo ya 33 kwa timu hizo kukutana ambapo 10 kati ya hizo Italia iliibuka kidedea huku Hispania wao wakishinda tisa na kutoa sare michezo 13. Hiyo pia itakuwa ni nafasi nzuri kwa Del Bosque kuangalia kiwango cha mshambuliaji wa Atletico Madrid ambaye ni mzaliwa wa Brazil Diego Costa kwa mara ya kwanza na kuona ni jinsi gani anaweza kufaa katika kikosi chake. Akiwa anaongoza katika La Liga msimu huu akiwa na mabao 19, Costa alichagua kuichezea Hispania badala ya Brazil na Del Bosque alimuita kwa mara kwanza katika mechi za kirafiki dhidi ya Equatorial Guinea na Afrika Kusini zilizochezwa Novemba mwaka jana. Hata hivyo ilibidi ajitoe baada ya kupata majeruhi na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji anayekipiga katika klabu ya Juventus ya Italia Fernando Llorente.

No comments:

Post a Comment