Tuesday, January 7, 2014

RAIS WA BRAZIL AMPASHA BLATTER.

RAIS wa Brazil, Dilma Rousseff amesisitiza kuwa taifa hilo litaandaa michuano ya Kombe la Dunia yenye mafanikio na kupuuza malalamiko ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwamba walianza maandalizi wakiwa wamechelewa. Rousseff ametoa kauli hiyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter na kudai kuwa taifa hilo linapenda soka na hawana budi kujivunia kuandaa michuano hiyo mikubwa. Rais huyo aliendelea kuandika kuwa mahitaji ya tiketi za michuano hiyo ni makubwa kuliko yaliyowahi kuandaliwa na nchi yoyote na hiyo inaonyesha mashabiki duniani kote wana imani na Brazil. Kauli ya Rousseff imekuja kufuatia rais wa FIFA Sepp Blatter katika mahojiano yake nchini Switzerland kuiponda Brazil kwa maandalizi ya taraibu ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment