MSHAMBUAJI wa kimataifa wa Ghana, Jordan Ayew anatarajiwa kuungana na kocha wa zamani wa zamani Herve Renard. Ayew ambaye ni mtoto zamani wa nguli wa soka wa Ghana Abeid Pele amehakikishwa muda mwingi wa kucheza na Renard katika klabu yake mpya ya Sochaux. Kinda huyo amejiunga na timu hiyo kwa mkopo akitokea katika klabu ya Olympique Marseille ambapo amekuwa akikosa muda wa kutosha wa kucheza. Renard amesema anaishukuru Marseille kwa kumuachia nyota huyo ili aweze kupata muda zaidi wa kucheza na kutimiza malengo yake ya kuwemo katika kikosi cha Ghana kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment