MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amethibitisha kuwa atashiriki sherehe za utoaji tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa mwaka ijulikanayo kama Ballon d’Or zitakazofanyika wiki ijayo. Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 anachuana na Lionel Messi wa Barcelona na Franck Ribery wa Bayern Munich katika tuzo hizo ambapo kumekuwa na tetesi kuwa anaweza asihudhurie tuzo hizo kutokana na kauli ya Sepp Blatter iliyokuwa ikimuunga mkono Messi. Hata hivyo nyota huyo akihojiwa mara baada ya timu yake kuitandika Celta Vigo kwa mabao 3-0, aliondoa uvumi huo na kubainisha kuwa atakuwepo jijini Zurich kuhudhuria utoaji wa tuzo hizo Januari 13. Ronaldo amesema atahudhuria pamoja na kwamba hajui kama ni haki kwake kushinda tuzo hiyo na kama akishinda sawa na akikosa ataendelea kujituma ili kuisadia Real Madrid kama kawaida.
No comments:
Post a Comment