MSHAMBULIAJI mkongwe wa klabu ya Udinese ya Italia, Antonio Di Natale ametangaza kuundika daluga zake mwishoni mwa msimu huu. Di Natale alitangaza uamuzi wake huo jana baada ya Udinese kupoteza mchezo wake dhidi ya Hellas Verona kwa kufungwa mabao 3-1. Nyota huyo amesema tayari ameshafanya uamuzi baada ya kuzungumza na familia yake na wakala huku akiwa na mpango wa kuifahamisha klabu haraka iwezekavyo kwamba ataachana na soka Juni mwaka huu. Di Natale ambaye anafikisha umri wa miaka 36 Octoba mwaka huu ameichezea Udinese kwa miaka tisa na kufunga mabao 182 katika mechi 359 alizoichezea timu hiyo katika mashindano yote huku mara mbili akimaliza kama mfungaji bora wa Serie A.
No comments:
Post a Comment