Monday, January 6, 2014

ROBSON HATIHATI KUCHEZA AUSTRALIA OPEN.

MATUMAINI ya mchezaji tenisi nyota kutoka Uingereza, Laura Robson kucheza michuano ya wazi ya Australia wiki ijayo yameingia dosari baada ya kuumia kifundo cha mkono wake wa kushoto katika michuano ya Kimataifa ya Hobart. Mwanadada huyo anayeongoza katika orodha za ubora wa mchezo huo nchini Uingereza wiki iliyopita alijitoa katika michuano ya ASB Classic kwasababu ya tatizo kama hilo. Robson mwenye umri wa miaka 19 alijitoa katika mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo wakati akiwa mbele ya Yanina Wickmayer wa Ubelgiji kwa 6-4 0-2. Tatizo hilo limekuwa sugu kwa mchezaji huyo ambaye pia alilazimika kujitoa katika michuano ya Kombe la Rogers Agosti mwaka jana kwa tatizo kama hilo. Michuano ya wazi ya Australia inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 13 jijini Melbourne.

No comments:

Post a Comment