Tuesday, January 14, 2014

RONALDO AKIRI KUFIKIRIA KUREJEA MAN UNITED.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amedai kuwa alifikiria kurejea Manchester United baada ya Rio Ferdinand kujaribu kumshawishi arejee katika usajili wa majira ya kiangazi. Ferdinand tayari alibainisha kumpigia simu nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kuhusu kurejea Old Traford kabla ya hajasaini mkataba mpya Santiago Bernabeu. Roaldo ambaye ametawadhwa kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or jana alithibitisha kuwa alikaa na kufikiria kwa karibu suala la kuijunga tena na United baada ya kufanya mazungumzo na Ferdinand. Ronaldo amesema alifikiria kuhusu United kwasababu bado wako katika moyo wake na ni timu ambayo amecheza kwa miaka sita na kutengeneza marafiki wengi. Nyota huyo pia akiri kuzungumza na Ferdinand kuhusu suala hilo kwasababu wamekuwa marafiki wa karibu sana na pia walikuwa majirani wakati bado anaishi Manchester.

No comments:

Post a Comment