MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amewaonya wapinzani wake kuwa timu yake ina uwezo wa kupambana na kuhakikisha inashinda taji la Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya timu hiyo kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kwa ushindi dhidi ya Aston Villa. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Wenger amesema ushindi huo ulikuwa mkubwa kwao ambapo katika kipindi cha kwanza walitawala kwa kumiliki mpira na kucheza pasi kama walivyozoea tofauti na kipindi cha pili ambapo ilikuwa ni mapambano zaidi. Wenger aliipongeza safu yake ya ulinzi kwa kufanya kazi kuhakikisha washambuliaji wa Villa hawatambi langoni mwao. Kocha aliendelea kudai kuwa ni jambo gumu kucheza wa mwisho kwasababu kila mtu anataka kukutizama kama utapoteza alama baada ya kila mpinzani kushinda mechi zao za mwishoni mwa wiki. Wenger amesema jibu pekee ambalo anaweza kuwapa ni kwa kushinda mechi yao na kuwasambazia ujumbe kuwa wapo hapo kwa ajili ya kushindana.

No comments:
Post a Comment