WACHUNGUZI nchini Ufaransa wamedai kuwa picha za video katika kamera iliyowekwa katika kofia gumu alilokuwa amevaa Michael Schumacher zinaonyesha kuwa alikuwa akiteleza katika mwendo wa kawaida wakati alipojikwaa katika jiwe na kuanguka. Mbali na hilo wachunguzi hao pia wamebaini kuwa dereva huyo wa zamani wa langalanga alikuwa mita nane pembeni ya barabara ya kawaida wakati akipata ajali na hakuonekana kupunguza mwendo aliokuwa nao. Schumacher alipata majeraha kadhaa ya kichwa baada ya kupata ajali hiyo Desemba 29 mwaka jana. Madaktari wamemuweka katika madawa mazito ya usingizi kutoka na kumfanyia upasuaji mara mbili ili kuondoa damu iliyovilia katika ubongo wake ambapo inadaiwa hali yake inatengemaa lakini bado hajaondoka katika hatari ya kupoteza maisha.
No comments:
Post a Comment