MWANARIADHA nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica, mwanadada Sherone Simpson ameliambia jopo la kamati ya nidhamu ya nchi hiyo kuwa hakutumia dawa zilizokatazwa michezoni kwa kudhamiria. Simpson ambaye alishinda medali ya fedha katika mbio za mita 400 kupokezana vijiti kwenye mashindano ya olimpiki yaliyofanyika jijini London anatuhumiwa kwa kukutwa na chembechembe za dawa hizo katika damu yake ambazo alipewa na mkufunzi wake Christopher Xuereb. Mwanadada alijitetea kuwa kosa lake kubwa ni kumuamini mkufunzi wake ambaye ndio alimtumbukiza katika matatizo hayo lakini haikuwa nia yake kutumia madawa hayo. Simpson pamoja na mshindi wa zamani wa rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 Asafa Powell wote walikutwa na chembechembe za dawa aina ya oxilofrine Juni mwaka jana.
No comments:
Post a Comment