KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Ivory Coast amefanikiwa kunyakuwa kwa mara ya tatu tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika inayotolewa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF. Toure anayekipiga katika klabu ya Manchester City ya Uingereza, aliwazidi John Obi Mikael wa Nigeria na Didier Drogba ambaye wanatoka nchi moja na kufikisha tuzo ya tatu sawa na Abeid Pele wa Ghana na Samuel Eto’o wa Cameroon. Akihojiwa mara baada ya tuzo hizo, nyota huyo alidai kuwa anafurahia kuwa mshindi lakini pia anampongeza mpinzani wake wa karibu Obo Mikael kwani na yeye alistahili tuzo hiyo. Mbali na Toure, Mohamed Abou Trika wa Misri naey alipewa tuzo hiyo akiwakilisha wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika huku kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Steven Keshi akipewa tuzo ya kocha bora wa mwaka.

No comments:
Post a Comment