Friday, January 10, 2014

RONALDINHO AONGEZA MKATABA MWINGINE NA ATLETICO MINEIRO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Ronaldinho amekubali kusaini mkataba mpya na klabu ya Atletico Mineiro baada ya kukataa ofa ya kwenda klabu ya Besiktas ya Uturuki. Mwezi uliopita Besiktas ilidai kuwa na nia ya kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 lakini wakakiri kuwa wanahitaji wadhamini zaidi ili kufikia kiwango cha mshahara cha mchezaji huyo. Nyota huyo wa zamani wa Barcelona na AC Milan alijiunga na Atletico Juni 2012 na kufanikiwa kushinda taji la klabu bingwa ya Amerika Kusini mwaka mmoja baadae. Ronaldinho amekuwa akionyesha kiwango kilichomfanya kupewa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2004 na 2005 hatua ambayo imepelekea kocha wa Brazil Luis Felipe Scolari kumuita katika kikosi chake.

No comments:

Post a Comment