WIKIENDI hii itakuwa muhimu sana kwa wale wanaofuatilia mpira wa kikapu nchini Marekani ambapo Chama cha Mpira wa Kikapu nchini humo, NBA kitawakutanisha wachezaji nyota wa upande wa Mashariki na wale wa upande wa Magharibi. Mechi hii huwa na upinzani mkubwa huku wachezaji wakipata nafasi ya kuonyesha umahiri wao ambao umewafanya kujulikana na kuwa maarufu duniani kote. Mbali na mechi lakini pande hizo mbili zikikutana huwa kunakuwa na maonyesho mbalimbali ikiwemo umahiri wa kuruka juu na kufunga yaani dunking na kutupa mitupo ya mbali yaani threethrow. Katika mchezo huo utashuhudia nyota mbalimbali wa upande wa mashariki wakiwemo LeBron James, Antony Davis, Carmelo Antony, Paul George, Kyrie Irving na wengineo huku upande wa magharibi ukiwa na nyota kama Kevin Durant, Stephen Curry, Blake Griffin, Kevin Love na Dwight Howard.

No comments:
Post a Comment