Thursday, February 13, 2014

MESSI AREJESHA MAKALI YA KUFUNGA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi ameendelea kurejesha makali ya ufungaji taratibu baada ya kuisadia timu hiyo kutinga fainali ya Kombe la Mfalme. Katika mchezo huo Messi aliifungia timu yake bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza kabla ya Real Sociedad kusawazisha bao hilo katika kipindi cha cha pili kupitia kwa Antoine Griezmann na kufanya Barcelona kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1. Bao hilo linamfanya Messi kufikia rekodi ya nyota wa zamani wa Barcelona Telmo Zarra ya mabao 335. Barcelona sasa itakutana na Real Madrid katika fainali ya michuano hiyo baada ya Madrid kuwasambaratisha mahasimu wao kutoka jiji moja Atletico Madrid kwa jumla ya mabao 5-0. Timu hizo zimeshakutana mara sita msimu huu ikiwa mara ya saba huku kila timu ikiwa imeshinda kombe hilo mara tatu.

No comments:

Post a Comment