Thursday, February 13, 2014

SARE YAMPA AHUENI WENGER.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa kikosi chake kingeweza kuondoka na alama zote tatu dhidi ya Manchester United jana lakini ameridhishwa na jinsi safu yake ya ulinzi ilivyocheza baada ya kipigo cha kudhalilisha walichokipata kutoka kwa Liverpool wiki iliyopita. Sare ya bila kufungana waliyopata dhidi ya United jana iliinyima nafasi timu hiyo kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza hivyo kuwaacha Chelsea wakiendelea kujitanua huko juu. Akihojiwa kuhusiana na mechi hiyo ya jana, Wenger amesema anadhani walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwani walipoteza baadhi ya nafasi chache muhimu walizotengeneza. Wenger aliendelea kudai kuwa anawapongeza mabeki wake kwani walifanya kazi kubwa ya kutorudia makosa waliyofanya katika mchezo dhidi ya Liverpool Jumamosi iliyopita. Arsenal bado wako katika mwezi mgumu kwani Jumamosi wanatarajiwa kuikaribisha Liverpool katika mchezo wa Kombe la FA kabla ya kuwakaribisha mabingwa wa Ulaya Bayern Munich katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani humo siku tatu baadae.

No comments:

Post a Comment