ROBINHO KUIKOSA ATLETICO MADRID.
MENEJA wa klabu ya AC Milan, Clarence Seedorf anaweza kulazimika kukosa huduma ya Robinho katika mchezo wa Serie A dhidi ya Bologna utakaochezwa Ijumaa na pia mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Atletico Madrid wiki ijayo. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil alipata majeraha ya msuli katika mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Napoli ambao waliambulia kichapo cha mabao 3-0 na kupelekea kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mbrazil mwenzake Kaka katika muda wa mapumziko. Robinho mwenye umri wa miaka 30 sasa anatarajiwa akufanyiwa vipimo ili kujua ukubwa wa tatizo lake na kuna hatihati ya kutokuwa fiti kwa wakati kwajili ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico utakaochezwa San Siro. Robinho ambaye pia amewahi kukipiga katika klabu ya Manchester City amefunga bao moja pekee katika mechi tano za Ligi ya Mabingwa alizocheza msimu huu.
No comments:
Post a Comment