KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Cesc Fabregas amemtaja meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kuwa mtu muhimu katika kazi yake ya soka. Fabregas mwenye umri wa miaka 26 alisajiliwa na Wenger kutoka katika timu ya vijana ya Barcelona akiwa na umri wa miaka 16 na haraka alionyesha kiwango kizuri katika timu ya vijana ya Arsenal kabla ya kucheza kwa mara ya kwanza timu ya wakubwa mwaka 2003. Kwa ujumla Fabregas amecheza Arsenal kwa miaka nane kabla ya kurejea Camp Noun na ingawa alifanyiwa kunyakuwa taji la FA pekee mwaka 2005 bado anadhani kocha huyo ni muhimu kwake. Wakati huohuo Fabregas sambamba na Wenger walimtetea kiungo Mezut Ozil ambaye mashabiki wamekuwa wakihoji juu ya kiwango chake kuporomoka hivi karibuni. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameshindwa kufunga bao katika mechi nane zilizopita za timu hiyo huku akishindwa kutengenza nafasi hata moja iliyozaa bao toka Desemba mwaka jana. Hata hivyo Wenger pamoja na Fabregas wamedai kuwa Ozil anajitahidi kuzoea mazingira ya Ligi Kuu nchini Uingereza anachohitaji ni muda kabla hajarudisha makali yake.

No comments:
Post a Comment